Wakazi mijini hatarini uchafuzi wa hewa

UCHAFUZI wa hewa umeendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya wananchi nchini Tanzania.Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuwa viwango vya juu vya uchafuzi vinakumba miji mikubwa kama Dar es Salaam, huku athari zake zikikumba hasa watoto, wajawazito, na watu wanaoishi katika maeneo yenye shughuli nyingi za viwanda na usafiri.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Health Effects Institute (HEI) ya mwaka 2025 inaeleza kuwa: “Uchafuzi wa hewa ni sababu kuu ya pili inayosababisha vifo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ikiwa na vifo takribani 294,000 mwaka 2021.” SOMA: Milioni 400 kukabiliana mabadiliko ya tabianchi
Aidha, tafiti zinaonesha kuwa “watoto katika maeneo ya Dar es Salaam wanakumbwa na dalili za magonjwa ya kupumua kama kikohozi, kupumua kwa shida, na pumu, kutokana na viwango vya juu vya PM2.5 na PM10.”
Ripoti nyingine ya Shirika la Afya Duniani (WH0) inasema: “Vifo 60 kwa kila watu 100,000 vinahusishwa na uchafuzi wa hewa wa ndani kila mwaka nchini Tanzania. ” Hali hii inatishia afya ya jamii na inaashiria umuhimu wa kuchukua hatua za haraka.”
Watafiti na wadau wa afya wanasisitiza kuwa serikali lazima iimarishe sheria za udhibiti wa uchafuzi wa hewa na kuhakikisha utekelezaji wake unafanikishwa. Kwa kufanya hivyo, Tanzania inaweza kupunguza athari za uchafuzi wa hewa https://www.instagram.com/reel/DHG915RqpMi/?hl=enna kulinda afya ya wananchi wake, huku ikiimarisha usalama wa mazingira kwa vizazi vijavyo.



