Watoto, wanawake wahanga usafirishaji binadamu

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Tanzania Relief Initiative (TRI) limesema zaidi ya asilimia 71 ya watoto wa kike na wanawake ni wahanga wanaofanyiwa usafirishaji haramu wa binadamu.

Mkurugenzi wa TRI, Edwin Mugambila jijini Dar es salaam kwenye semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari ya namna ya kuripoti matukio ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Advertisement

” Usafirishaji haramu wa binadamu ni mmoja wa uhalifu unaovuka mipaka ambao unatishia dunia kwa sasa na wahanga wakubwa ni watoto wa kike na wanawake zaidi ya asilimia 71 na maeneo yaliyoathirika zaidi  ni maeneo ya kijijini,”

“Baada ya waandishi kupata mafunzo hayo watakuwa jicho kwa jamii kwa kuibua  visa hivyo vya usafirishaji haramu wa binadamu  kwa kuhabarisha jamii na kuhakikisha ile mitandao yote  ya hao wanaofanya huo uhalifu inakatwa kanisa na kufanya jamii yetu kuwa salama dhidi ya wanaofanya vitendo vya usafirishaji haramu,” amesema  Mugambila.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Taasisi ya Hans Seidel, Frank Gollwitzer amesema semina hiyo na mada zinazotolewa kwa waandishi hao zitawapa uelewa mpana zaidi na kuwapa taarifa zaidi juu ya usafirishaji huo haramu wa binadamu.

Kwa upande wao waandishi walioshiriki semina hiyo ,Elias Julius na Philip Mwihava wamesema semina hiyo imewapa mwangaza ni namna gani watakavyoripoti habari za usafirishaji haramu wa binadamu na hivyo watawafichua kwa jamii wanaofanya hivyo.