Watoto wanne familia moja wateketea kibanda cha mganga kikiungua

WATOTO wanne wa familia moja wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada kibanda cha mganga wa kienyeji walipo kuwa kuungua moto.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Richard Abwao amesema watu wengine saba wamekimbizwa hospitali na jeshi la polisi lina mshikilia mganga huyo anayedaiwa kuwasha moto katika kibanda hicho kwa lengo la kuondoa nuksi katika familia.

Kamanda amesema kuwa watoto hao waliungua wakati wakigombania kutoka nje ya kibanda baada ya moto kuzidi. Moto huo ulikuwa ukiwaka kuzunguka kibanda walichokuwemo pamoja na watu wengine ndani ya familia.

“Kulikuwa na watu 20 kwenye kibanda kilichowashwa moto na mganga huyo aliyewapa sharti la kutoka mmoja mmoja baada ya moto kuwashwa, hata hivyo ulizidi na kushindwa kutoka na kusababisha watoto hao kuungua na kufariki,’ amesema.

Amesema tayari mganga anayetuhumiwa kuhusika katika tukio hilo amekamatwa na upelelezi wake unaendelea.
Kwa mujibu wa taarifa wa Diwani wa Kigwa, Bakari Kabata amesema watoto hao waliofariki wana umri wa miaka 15 na wanne waliopoteza maisha ni wa familia moja.

Akielezea tukio amesema mwenyeji wa mji huo, alimuita mganga kwa mambo ya kimila, akimtaka kumuondolea mkosi kwenye nyumba yake.

Amesema kuwa mama wa familia hiyo ni miongoni mwa majeruhi saba ambao wamelezwa katika Hospitali ya Omulinga ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora,Kitete.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x