Watu 13 wapoteza maisha ajali ya treni India

WATU 13 wamepoteza maisha na wengine zaidi 50 kujeruhiwa baada ya treni mbili kugongana Kusini Mashariki mwa India, maafisa wamesema leo.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili jioni kati ya miji ya Alamanda na Kantakapalle katika jimbo la Andhra Pradesh.

Uchunguzi wa awali uligundua kuwa “makosa ya kibinadamu” yalisababisha mgongano huo, wizara ya reli ilisema katika taarifa yake.

“Abiria 13 wameuawa na wengine 50 wamejeruhiwa. Shughuli za uokoaji zinaendelea,” ofisa mkuu wa serikali eneo la Nagalakshmi S. aliwaambia waandishi wa habari.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button