Watu 400 kushiriki kongamano la muziki Dar

WATU 400 tayari wamejisajili kushiriki Kongamano la Pili la Kimataifa la Muziki la ACCES lililopangwa kufanyika Novemba 9 hadi 11 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Oktob a 18,2023 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Kedmon Mapana amesema Kongamano hilo litashirikisha watu zaidi ya 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

“Serikali tunafarijika Kongamano hili litatupatia fedha nyingi za kigeni, watakaa mahotelini, watatengeneza ‘network’, Basata tunalipa baraka kongamano hili kwa mikono miwili.

Advertisement

” Amesema Mapana

Aidha, kwa upande wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Music in Africa Eddie Hatitye amesema mbali na wanamuziki kutoka mataifa mbalimbali kutumbuiza pia kutakuwa na watoa mada zaidi ya 40 kutoka Afrika na duniani kote, ambao wataangazia mambo muhimu kwenye tasnia ya muziki kitaifa na kimataifa, na namna ya kuukuza, kukuza ujuzi na fursa kwa wadau katika tasnia ya muziki Afrika.

Amesema, kongamano hilo linafanyika kila mwaka kwenye miji mbalimbali ndani ya Afrika, na kutoa fursa kwa wanamuziki kukuza na kujenge uwezo wao na kutumbuiza mbele ya hadhira iliyosheheni wageni wa kitaifa na kimataifa, ikiwemo waandaaji wa matamasha, mapromota, mawakala wa muziki, lebo za kurekodi muziki na hadhira yenye ushawishi mkubwa.

“Pia wageni watapata fursa ya kutembelea vituo mbalimbali vya tasnia ya muziki Tanzania,”amesema.

Amesema kongamano hilo ni bure kwa Waafrika ambao watataka kushiriki na ili upate nafasi ya kuhudhuria wanatakiwa kujisajili kwanza kupitia tovuti rasmi.

Miongoni mwa watu mashuhuri wataoshiirki kwenye kongamano hilo nimwanamuziki na mjasiriamali wa Afrika Kusini Sho Madjozi atakayefanya mahojiano na Heather Maxwell wa Sauti ya Amerika, wakati msanii na mtayarishaji wa muziki wa bongo flava kutoka Tanzania Marioo atatoa mada kwenye mkutano huo.

Amesema, ACCES pia itaandaa mijadala ya kina kuhusu usimamizi wa haki za muziki, ujasiriamali wa muziki, uchapishaji wa muziki, branding, ziara za muziki, ushirikiano na teknolojia katika tasnia ya muziki.

Baadhi ya wazungumzaji mashuhuri ni pamoja na mwanzilishi wa SymphonyoS Chuka Chase (Marekani), mwanzilishi wa Roxanne Sonia Boton-Gboh (Ufaransa), Ofisa Maendeleo wa kimataifa wa SACEM Afrika Akotchayé Okio (Ufaransa) na Mkurugenzi Mkuu wa Sony Music Publishing Afrika Kusini, Rowlin Naicker (AfrikaKusini).

Wengine ni mwanzilishi wa Singeli Festi, Masudi Kandoro (Tanzania), Mwanzilishi wa SaveFi Tech Ebenezer Akachukwu (Nigeria), Mwanzilishi Mwenza wa Vth Season, Raphael Benza (Afrika Kusini), Mwanzilishi wa SlikourOnLife, Siya Metane (Afrika Kusini) na Meneja Mkuu EMPIRE, Moody Jones (Marekani).

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *