Watu saba wafa maji wakivuka mto

KATAVI: WATU saba kati ya 14 waliyokuwa wakisafirisha magunia ya mpunga kwa kutumia mtumbwi katika bonde dogo la Kitongoji cha Luguya kilichopo Kijiji cha Mwamapuli Halmashauri ya Mlele mkoani Katavi wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliyokuwa wakisafiria kupinduka.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/mafuriko-yauwa-watatu-familia-moja/

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi, Inspekta Lilian Wanna amesema tukio hilo limetokea Mei 24 mwaka huu majira ya saa 12 jioni.

Ameeleza kuwa ajali hiyo iliwakuta watu hao walipokuwa wakitoa mazao yao shambani baada ya kuyavuna na kuyaleta kijijini.

Ameongeza kuwa wanaendelea na uokoaji licha ya kuwa bonde hilo kuwa na changamoto ya uwepo wanyama wakali kama Mamba na Viboko.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7bpPEvOj7e/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwanamvua Mrindoko amefika kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto katika uokoaji.

Habari Zifananazo

Back to top button