Watuhumiwa 23 mbaroni vitendo kinyume na maadili

JESHI la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watuhumiwa 23 mkoani humo kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ubakaji na mengine.

Akizungumza leo mkoani Mtwara alipotoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara SACP, Issa Seleimani amesema katika watuhumiwa hao waliyokamatwa wakiwemo hao waliyojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, walitenda tukio hilo Januari 2025 katika nyumba ya kulala wageni.

Amewataja kwa majina watuhumiwa hao kuwa, Dickson Paul (27) anayejishughulisha na masuala ya ujasiliamali mkazi wa mkuti chini machinjioni wilaya Masasi na Mohamed Ally (34) mwalimu katika shule ya msingi nanyani iliyopo Wilaya ya Mtwara.

Advertisement

Watuhumiwa wengine akiwemo Ally Salum (53) mlinzi kwenye kampuni ya kiwango Security katika kiwanda cha kuzalisha saruji (Dangote) anashikiliwa kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kike (10) mwanafunzi wa darasa la nne ambaye ni mkazi wa magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani.

‘’Jeshi la polisi linaendelea kuwasisitiza wananchi kuwa jukumu la malezi na ulinzi wa mtoto ni la kila mtu na siyo taasisi moja pekee hivyo wazazi wanakumbushwa kulipa kipaumbele suala la ulinzi na malezi kwa kuwa kila mtoto ana ndoto ya kesho bora’’amesema Suleimani

Katika hatua nyingine Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu Januari 2025 ilimhukumu kifungo cha miaka 90 na miezi miwili jela Salum Yohana (54) mkazi wa kijiji cha mnazi mmoja wilayani humo kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kupatiana na mbegu na majani ya mimea ya dawa za kulevya aina ya bhangi.

Hata hivyo kwa upande wa usalama barabarani, jeshi hilo limefanikiwa kukamata jumla ya makosa ya usalama barabarani 4,247 kati ya hayo makosa ya magari 3,133 na makosa ya babaji na pikipiki 1,114.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *