Watumishi 34 washinda rufaa

TUME ya Utumishi wa Umma imepokea rufaa na malalamiko 108 ya watumishi wa umma dhidi ya waajiri, mamlaka za ajira na mamlaka za nidhamu katika utumishi wa umma.

Mkutano wa tume ulioongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Hamisa Kalombola ulipitia kujadili na kuamua rufaa na malalamiko ya watumishi yaliyowasilishwa.

Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, John Mbisso amesema tume ilitoa uamuzi wa rufaa 93 na malalamiko 15.

Mbisso amesema rufaa za watumishi 34 zilikubaliwa, hivyo watumishi hao wanatakiwa kurudishwa kazini na kupewa stahiki zao.

Amesema rufaa tisa zilikubaliwa kwa masharti kwamba, mamlaka za nidhamu hazikuzingatia sheria na kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria.

Mbisso amesema rufaa 38 zilikataliwa, kwani zilithibitisha watumishi walituhumiwa kihalali na mchakato wa kuwapa adhabu ulizingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo.

Amesema rufaa 10 zilitupwa kwa kuwa zilikuwa zimewasilishwa kwenye tume nje ya muda wa kikanuni wa siku 45.

Mbisso alisema kati ya malalamiko 15 ambayo yaliwasilishwa na watumishi kutokana na waajiri kuchelewesha stahiki zao, sita yalikubaliwa, sita yalikataliwa na matatu yalitupwa kwa kuwa yaliwasilishwa nje ya muda wa kikanuni wa mwaka mmoja.

Amesema tume inawakumbusha watumishi wazingatie sheria ili kujiepusha na vitendo vinavyoashiriria ukiukwaji wa maadili, hali inayoweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kinidhamu au za kijinai.

Mbisso amesema rufaa nyingi zilizowasilishwa zilihusu kukiuka maadili, utoro kazini, kughushi vyeti na kutoa taarifa za uongo, uzembe wa kushindwa kutekeleza majukumu na wizi wa mali za umma.

Amesema malalamiko mengi yaliyowasilishwa yalihusu watumishi kutolipwa stahili zao na waajiri ikiwemo mishahara, stahili za uhamisho, posho, pia kutopandishwa vyeo na kuchelewa kupandishwa vyeo pamoja na kuondolewa kwenye utumishi, kinyume cha sheria.

Mbisso ametoa mwito kwa waajiri, mamlaka za ajira na mamlaka za nidhamu wazingatie sheria wakati wa kushughulikia masuala ya ajira na mashauri ya nidhamu ya watumishi ili haki si tu itendeke, bali ionekane inatendeka.

Ofisa Sheria katika Tume ya Utumishi wa Umma, Hussein Mussa amesema ni hasara kubwa kwa mtumishi kupoteza haki za ajira kwa kufukuzwa kazi, kushushwa cheo na kushushwa mshahara asilimia 15 kwa miaka mitatu au kupewa onyo, karipio na adhabu nyingine.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button