Watumishi sasa mshindwe wenyewe

ARUSHA: Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Ephraim Mafuru amesema michezo mahali pa kazi ina umuhimu mkubwa kwasababu inasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi .
Mafuru ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akiagana na timu ya michezo ya AICC inayokwenda Dodoma kushiri kwenye mashindano ya 52 ya michezo ya Taasisi za Umma na Mshirika Binafsi SHIMUTA inayoanza kesho
“Nawapongeza kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha taasisi yetu ya AICC katika michezo ya SHIMUTA, ushiriki wenu na uwepo wenu katika michezo hii ni kielelezo tosha ya kwamba tuna dhamira ya kweli kutekeleza sera za Serikali ya awamu ya sita na hasa katika suala la michezo,”amesema
Amesisitiza kuwa AICC imedhamiria kuboresha afya ya mwili na akili za wafanyakazi na kudumisha umoja ndani ya Kituo na kujenga mahusiano kati ya watumishi wa AICC na taasisi nyingine za serikali.
Kwa upande wake kiongozi timu ya AICC yenye washiriki 11, Zamda Masoud alimshukuru Mafuru kwa kuiwezesha timu hiyo kushiriki kikamilifu katika michezo hiyo.
Michezo ya SHIMUTA hufanyika kila mwaka na kuwakutanisha watumishi wa taasisi za umma na mashirika binafsi kushiriki katika mashindano ya michezo mbalimbali.



