Watumishi TSN walivyojinafasi CRDB International Marathon

DAR ES SALAAM: WATUMISHI wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Asha Dachi ni miongoni mwa wanamichezo walioshiriki mbio za CRDB Bank International Marathon 2025 zilizofanyika kwenye viwanja vya Farasi, maarufu kama ‘The Greens’, Oysterbay, jijini Dar es Salaam leo Agosti 17, 2025.

Akizungumza kwenye mbio hizo, Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson ambaye likuwa mgeni rasmi, alitoa wito kwa washiriki wa mbio hizo wazitumie kama fursa za kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Amesema chama cha riadha kisaidie pia mbio nyingine zinakuwa kubwa za kimataifa, kwani zitasaidia kuongeza idadi ya watalii wengi nchini hivyo zitachechemua uchumi wa nchi.




