Watumishi wa magereza Bukoba wagaiwa majiko

BUKOBA: Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamezindua zoezi la kugawa majiko na mitungi ya gesi 486 kwa watumishi wote wa magereza manane Bukoba ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono sera ya serikali ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania wote mpaka ifikiapo mwaka 2034.
Akizindua zoezi hilo kwa watumishi wa 99 wa magereza ya Bukoba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Lucas Charles alisema kuwa serikali imeagiza magereza zote nchini kutumia nishati safi ya kupikia na magereza zote nchini zimetekeleza zoezi hilo.
Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha watanzania wote wanaoishi vijijini na mjini wanatumia nishati safi ya kupikia kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2034 na kudai kuwa kwa sasa mwitikio ni mkubwa wa wananchi wanaotumia nishati safi.

Meneja usaidizi wa Kiufundi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Emmanuel Yesaya alisema kuwa serikali kupitia kwa wakala huo imetenga Sh bilioni 35 kwa ajili ya kusambaza majiko na mitungi kwa watumishi wote wa magereza nchini, ujenzi wa miundo mbinu ya nishati safi ya kupikia kwa magereza zote nchini usambazaji wa mkaa mbadala wa kupika katika magereza zote tani 850, pamoja na ununuzi wa machine 61 za kuzalisha mkaa mbadala wa kupikia.

Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha mazingira yanaalindwa kwa nguvu zote, kuboresha afya za watanzania huku wakiokoa muda wa kufuata kuni na mkaa na badala yake kutumia muda muchache katika kuandaa chakula ,na muda mwingine utumike kufanya kazi nyingine za uzalishaji .
Ametoa wito kwa watumishi wote walionufaika na majiko hayo kuhakikisha wanakuwa sehemu ya hamasa kwa jamii ili kupitia kwao kiwango na idadi ya wananchi wanaotumia nishati safi iweze kuongezeka kwa kasi.
Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Heron Noberth alisema kuwa tayari magereza zote za mkoa wa Kagera wanatumia nishati safi ya kupikia tangu walivyosaini mkataba na serikali na utekelezaji wake uliaanza January 2025