Wawili waboresha maisha zawadi za mil 12.5/-

DAR ES SALAAM: WATANZANIA wameendelea kuboresha maisha yao kwa namna tofauti kupitia kampeni mbalimbali baada ya wawili kujishindia zawadi tofauti zinazokwenda kuongea thamani halisi ya maisha yao.
Habiba Ally na Alpha Isack, ni miongoni mwa waliokutana na fursa hiyo leo Julai 1, 2025 baada ya kujishindia bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 12.5 kufuatia ushiriki wao wa kampeni ya ununuzi wa vyakula migahawa ya KFC na Pizza Hut.
Washindi hao walitangazwa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni maalum iliyozinduliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Hisense.

Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa KFC, Lyse Mosha, alisema kampeni hiyo ilihusisha wateja wanaofanya ununuzi wa chakula ambapo kila mlo uliowekwa kwenye mfumo wa promosheni uliwapa nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.
“Tunaamini kila mteja anayechagua mlo wetu anatuamini. Lengo letu si tu kuuza chakula, bali pia kushiriki katika safari ya maisha yao,” alisema Mosha.
“Sikutarajia hata kidogo. Nilikwenda tu kununua chakula kama kawaida. Leo hii napata mamilioni ya zawadi kwa sababu ya kuwa mteja wa KFC,” alisema Habiba
Kwa upande wake, Alpha Isack, ambaye ni mteja wa Pizza Hut, alisema huduma za mgahawa huo zimekuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku, lakini hakutegemea kwamba kununua chakula kungempa fursa ya kubadilisha maisha yake.

Mwakilishi wa kampuni ya Hisense,Kalbe Husein, alisema ushirikiano wao katika kampeni hiyo unalenga kuonesha kuwa hata shughuli ndogo kama ununuzi wa mlo wa kila siku inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya mtu.
“Hisense inaamini katika nguvu ya teknolojia, chakula na burudani katika kuboresha maisha ya watu. Ushindi huu ni mfano halisi,” alisema.



