Wawili watiwa mbaroni uvuvi haramu feri

Kilo 980 za samaki zadakwa

JESHI la Polisi Kikosi cha Wanamaji Dar es salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Mifugo kimekamata kilo 980 za Samaki zilizokuwa ndani ya boti ynye usajili ndani Z Z. 103585 jina Mv Maedra.

Katika taarifa iliyotolewa leo Januari 24, 2023 na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji (T) Dar es Salaam, ACP Moshi Sokoro kwa vyombo vya Habari, inasema kuwa Januari 12 majira ya asubuhi katika eneo la Samaki Ferry walifanikiwa kukamata kilo hizo za Samaki wanaosadikiwa kuvuliwa kwa baruti.

“Katika operesheni ya pamoja ya kuzuia uvuvi haramu na makosa mengine ya kijinai tulifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili wakiwa na Samaki hizo, taratibu za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani zinaendelea. “Amesema na kuongeza

“Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru na kutoa pongezi kwa wananchi wote ambao wanachukia uhalifu na linawaomba waendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahalifu hao.”Amesema

Aidha, amesema pia Jeshi la Polisi linaendelea kutoa onyo na kwamba halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayejihusisha na uvuvi haramu pamoja na makosa mengine ya kijinai

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x