Waziri Kapinga: Kiwanda cha vifungashio kitachochea ajira

DAR ES SALAAM; WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema uanzishwaji wa kiwanda kipya cha kutengeneza vifungashio unaofanywa na Kampuni ya SBC Tanzania Ltd kutachochea ajira kwa vijana mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

Waziri Kapinga ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda  cha  Kampuni ya SBC Tanzania Ltd inayozalisha pia vinywaji vya Pepsi na kuelezwa kuwa kampuni hiyo  inatekeleza mpango mkubwa kuanzisha kiwanda kipya cha kutengeneza vifungashio vya plastiki jijini Dar es Salaam  na inatarajia kufungua  tawi mkoani Dodoma.

Akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Aristides Mbwasi, Waziri Kapinga ameeleza kuwa uanzishaji wa kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya plastiki hapa nchini ni hatua muhimu itakayopunguza utegemezi wa kuagiza malighafi hiyo kutoka nje, kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ajira  kwa vijana wengi.

Amesisitiza kuwa  wizara yake  itahakikisha inasimamia sera zinazochochea ukuaji wa viwanda mama, ili kuimarisha mnyororo wa thamani na kusaidia teknolojia zinazozalisha bidhaa bora kwa soko la ndani na nje.

Amebainisha kuwa ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya mradi huo wa SBC na amesema kuwa ujenzi wa tawi la Dodoma utasaidia kusogeza bidhaa karibu na walaji na kuimarisha uchumi wa makao makuu.

Naye Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBC, Foti Nyirenda, amesema kuwa hatua hizo za upanuzi  wa kiwanda cha Dar es Salaam na ufunguzi wa tawi jipya la Dodoma zitafungua fursa nyingi za ajira kwa Watanzania na utaongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa nchi nzima.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button