Waziri Mkuu aagiza wakimbiza mwenge kufichua maovu

WAKIMBIZA Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 wametakiwa kufichua maovu, vitendo nyote vya ubadhilifu wa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ili Serikali ifanyie kazi.

Akizungumza leo mkoani Mtwara katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa uliyofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni wajibu wa kila mmoja wao kulitekeleza jukumu hilo kubwa, muhimu na nyeti kwa taifa.

“Ni wajibu wa kila mmoja wenu kulitekeleza jukumu hilo kubwa, muhimu na nyeti kwa Taifa letu viwango nyenu vinazingatiwa na sisi tunawaamini kama mtachapa kazi.

”amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mmoja wao kulitekeleza jukumu hilo kwa bidii, weledi, nidhamu, uadilifu pamoja na maalifa ya hali ya juu.

Amesema kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru waende wakaangalie miradi hiyo kupitia hayo yote aliyoyaeleza kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya utekekezaji lakini kumekuwa na baadhi ya watendaji kuhujumu miradi ya maendeleo.

Hata hivyo waandae taarifa yao na kutoa mapendekezo kwani Serikali italifanyia kazi lakini pia kufichua vitendo vyote hivyo vya ubadhilifu wa fedha za miradi ya Umma bila kuwa na woga wowote ili Taifa liweze kusonga mbele.

Mwenge wa Uhuru huo utapita kwenye Mikoa 31 na Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kipindi hicho chote utafanya kazi ya kuhamasisha amani, Umoja, upendo na mshikamano wa Kitaifa pamoja kuwahimiza Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 inasema “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”,

Habari Zifananazo

Back to top button