Waziri Mkuu aanza ziara Songwe

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Februari 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songw,e ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la Hospitali ya wilaya ya Songwe.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ,ambapo halmashauri inatarajia kukamilisha mradi huu Machi 31, 2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo tayari vifaa vyake vimepokelewa.

Ujenzi katika hospitali hiyo inahusisha ujenzi wa majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, mionzi, maabara, ufuaji, famasia, utawala na jengo la mama na mtoto, ujenzi wa wodi tatu za magonjwa mchanganyiko.

 

Majengo mengine ni jengo la Huduma ya dharula na Nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la Upasuaji, jengo la Uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za Upasuaji (wanaume na wanawake)

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan amehakikisha hakuna eneo katika nchi hii ambako hapajatekelezwa miradi ya huduma za jamii kaunzia ngazi ya mkoa hadi kijiji.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x