Waziri Mkuu kufungua mkutano mkuu TAHOSSA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 12 anafungua mkutano Mkuu wa 19 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania(TAHOSSA) jijini Dodoma.
Mkutano huo unatoa fursa kwa wakuu wa shule kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka mzima na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini.
Kaulimbiu ya Mkutano huo ni “TEHAMA ni ufunguo katika kutekeleza mitaala na kutengeneza fursa za ajira Tanzania.”

Habari Zifananazo

Back to top button