Wenje awachana viongozi wanaosema wako tayari kufa

Aiwata waoga, atupa dongo CHADEMA

KAGERA: KADA wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye sasa ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ezekia Wenje, ametoa onyo kuhusu hatari ya kuwa na kiongozi wa chama cha siasa anayejinasibu kuwa yuko tayari kufa, na kusema kuwa kiongozi wa aina hiyo hana sifa za kuongoza Taifa.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM uliofanyika leo mkoani Kagera, Wenje amesema kauli kama hizo ni ishara ya kukata tamaa na kukosa dira ya kweli ya uongozi.

“Ni hatari sana kuwa na kiongozi wa chama cha siasa anayesema yuko tayari kufa. Kiongozi aliye tayari kufa ni kiongozi aliyekata tamaa kwa sababu hakuna matumaini kwenye kifo,” amesema Wenje.

Wenje amesisitiza kuwa kiongozi wa kweli ni yule anayethamini maisha yake na anayetumia hoja na sera kujenga Taifa, badala ya kutoa matamko ya vitisho au ya kushangaza.

Aidha, amekosoa uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kususia uchaguzi mkuu ujao, akidai kuwa chama hicho kilijiondoa kwa hofu ya kushindwa kwenye uwanja wa ushindani wa kisiasa.

“Biblia inasema Mungu hafanyi kazi na watu waoga. Watu waoga wanaokimbia uchaguzi licha ya mapendekezo na maombi yao kufanyiwa kazi, huo si uhodari wala ushujaa,” amesisitiza Wenje.

Pia Wenje ameongeza kuwa sababu zinazotolewa na CHADEMA za kutoshiriki uchaguzi hazina msingi, kwa kuwa mapendekezo mengi ya chama hicho yaliwasilishwa kwa Serikali ya Awamu ya Sita na yalizingatiwa.

Katika hatua nyingine, Wenje ametoa pongezi kwa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne iliyopita, hususan katika kujenga mazingira ya maridhiano ya kisiasa, kuanzisha mabadiliko ya sheria za uchaguzi, na kuweka msingi wa mazungumzo ya wazi kati ya Serikali na vyama vya siasa.

“Tumeona CHADEMA wakialikwa Ikulu mara kwa mara kwa ajili ya mazungumzo. Hili halikuwahi kutokea nyuma. Huu ni ushahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imefanya kazi kubwa ya kujenga daraja la maelewano,” ameongeza Wenje.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $100 to $500 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily 💵$20k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…

    Here is I started.→→→→→→→→→ https://Www.Works6.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button