WHO yakabidhi vifaa vya afya Kagera

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wamekabidhi vifaa vya afya kwa Halmashauri za Biharamulo na Muleba vyenye thamani ya Sh milioni 112.
Mkurugenzi mkazi wa mwakilishi wa shirika hilo, Dk Galberth Fadjo alisema kuwa shirika limeona jitihada za Serikali kwa namna linavyochukua hatua za haraka juu ya kudhibiti magonjwa yenye nguvu kama Marbug yasisambaze zaidi na kuhakikisha wanaopata madhara au ugonjwa wanarudi katika hali zao haraka bila kuleta madhara.
Akitoa mfano wa mlipuko wa ugonjwa huo hatarishi katika mkoa wa Kagera Wilaya ya Bukoba mwaka 2023 na wilaya ya Biharamulo mwaka 2024 namna serikali ilivyopambana bila kuathiri shughuli nyingine na wakaweza kurejesha hali katika jamii, kuwa huo ni mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine zinazokabiliana na majanga.

Alisema WHO itaendelea kukabiliana na dharura kwa uharaka katika kupambana na magonjwa ya mlipuko huku akitoa wito kwa mamulaka kutumia vifaa hivyo kutoa elimu ya kiutaalamu kwa watakaovitumia na kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kupambana na magonjwa ya mlipuko .
Mkurugenzi wa dharura na maafa kutoka wizara ya Afya alisema kuwa vifaa vilivyopokelewa ni vitanda vya kisasa vya kulaza wagonjwa,machine za kusafiisha mashuka,stendi za kuwekea dawa,ndoo za kuhifadhi maji na Kufanyia usafi katika vituo vya afya pamoja na vifaa vya kufanya uchunguzi wa kina.

Alisema kuwa hii ni sehemu kurejesha hali huku akidai kuwa tayari ugonjwa huo umewapa Mafunzo mbalimbali ambapo wizara ya Afya imejifunza kutoa elimu kwa wananchi kutoa taaarifa ya dharura pale wanapoona ugonjwa usio wa kawaida, kuimarisha utayari ,kushirikisha jamii pamoja na kuunganisha Wadau katika kudhibiti
Alisema kuwa vifaa vilivyotolewa vitaongeza ujuzi na utendaji kazi kwa wataalamu wa afya mkoani Kagera ambapo amelishuru shirika la WHO kwa utayari na usaidizi mzuri wa katika kipindi chote ambacho nchi ya Tanzania na mkoa wa Kagera walipokumbwa na mlipuko Wa ugonjwa huo.
Alitoa wito kwa halmashauri za mkoa wa Kagera kutenga bajeti ya ndani kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yanayojitokeza kwa dharura na kudai kuwa Mpaka sasa tayari wamekuwa na uzoefu juu ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Steven Ndaki alitoa wito kwa wataalamu kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa na kuongeza ujuzi wa kuvitumia pamoja na kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo bila kujali kama Kuna ugonjwa au hakuna ugonjwa
Alisema mkoa wa Kagera utaendelea kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na dharura zote za mlipuko kutoka na mkoa huo kuwa hatarini kwa kupakana na nchi nyingi ambazo zinaongeza uhatarishi wa magonjwa ya mlipuko.



