Wilaya ya Tanganyika kupanda zaidi ya miti mil. 3

Wilaya ya Tanganyika kupanda zaidi ya miti mil. 3

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi, imepanga kupanda miche ya miti ya matunda na mbao milioni 3.5, ikiwa ni kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika.

Akizindua shughuli hiyo eneo la Mpanda Kati, Kitongoji cha Mchakamchaka, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, alisema wameamua kufanya hivyo kama sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya uhifadhi wa mazingira.

Alisema kutokana na shughuli za kibinadamu, yapo baadhi ya maeneo miti imepungua, hivyo namna pekee ya kuirejesha ni kuhamasisha wananchi, taasisi na vyama vya msingi washiriki upandaji miti.

Advertisement

Mwenyekiti wa chama cha msingi (AMCOS) Mpanda Kati, Philbert Ngula, alisema malengo waliyojiwekea ni kila mwanachama kupanda miche 200 na kupitia mashamba ya pamoja ya AMCOS zaidi ya miche 30,00 inatarajiwa kupandwa, huku kila mwananchi akitakiwa kupanda angalau miche 50.

Mwakikishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Ambwene Yona, ambaye ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano, alisema mkakati mwingine waliojiwekea ni kila taasisi ya umma kupanda miti isiyopungua 1000, hiyo ikiwa ni kuhakikisha Tanganyika inabaki ya kijani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *