Wizara ya Elimu, Korea Kusini kuimarisha mafunzo ya STEM

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itashirikiana na Korea Kusini katika kuimarisha mafunzo ya Sayansi Teknolojia Uhandisi na Hesabu (STEM).
Hayo yamebainishwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika Dodoma ambapo washiki wa kikao wamejadiliana juu ya umuhimu wa kuanzisha sera ya elimu ya (STEM) yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati pamoja na maendeleo ya kitaaluma kwa walimu.

Programu hiyo imeanza kutekelezwa katika mikoa ya Simiyu na Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wataalamu kutoka Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais- Tamisemi na ujumbe kutoka Korea ulioongozwa na Profesa Nam Hwa Kang, kutoka Korea National University of Education (KNUE).



