Wizara yajivunia usawa uwekezaji wa kiuchumi

WIZARA ya Nishati imeeleza inajivunia jitihada zinazofanyika kulinda haki usawa na kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia nishati ya umeme na nishati safi ya kupikia.

Haya yamejiri kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025, yenye kaulimbiu “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”

Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema hayo alipoeleza namna Wizara ya Nishati inakwenda kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

“Tumepeleka umeme kwenye zaidi ya Vitongoji elfu 33, lakini kupitia nishati safi ya kupikia kupitia programu mbalimbali tumepeleka mitungi takribani laki 4020, majiko banifu laki 2 pamoja na majiko ya umeme,” amesema Kapinga.

Ameeleza kuwa jitihada zote za serikali katika uwekezaji sekta ya nishati hususani nishati safi ya kupikia zinalenga kuboresha ustawi wa mwanamke na kuongeza thamani yake katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika jamii.

Aidha, Kapinga amesema kuwa kupitia Sera ya Elimu Bure kumekuwa na ongezeko la dadi ya wanafunzi wa kike mashuleni, aidha uboreshaji katika sekta ya afya umewafanya wanawake wapate uhakika wa kuendelea na shughuli za uzalishaji kutokana na upatikanaji wa matibabu sahihi.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa tuzo ya Golkeeper ambayo imetambua mchango katika kupungiza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua kwa asilimia  80 na Vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa kila vizazi 1,000.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button