Wizara yatahadharisha uwepo wa corona

DODOMA: Wizara ya Afya imetoa tahadhari kuhusu ongezeko la visa vya magonjwa ya mfumo wa kupumua kama maambukizi ya mafua makali, kipindupindu na COVID-19.
Taarifa iliyotolewa leo jiji Dodoma na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Maghembe imeeleza kuwa magonjwa yanaibuka kipindi cha Novemba na Aprili.
Amesema magonjwa yote huambukizwa kupitia njia ya kukohoa, kupiga chafya, au kuzungumza, na kwa kugusa sehemu zilizochafuliwa
Ameeleza kuwa dalili zake ni pamoja na homa kali, kikohozi, maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, mafua, koo, na uchovu
 

Wizara inashauri umma kuchukua hatua za kinga kwa kufunika pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafyakuosha mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji yanayotiririka au sanitizer.

“Epuka maeneo yenye watu wengi, vaa barakoa ikiwa una dalili au katika maeneo yenye watu wengi, fanya usafi wa kibinafsi na wa kimazingira, na endapo mtu atagubdulika na tatizo awahi kituo cha afya hivyi wananchi wameonywa kuacha kujitibu, hasa kwa kutumia dawa za maumivu bila ushauri wa daktari.

Aidha pia ameonya uwepo wa homa ya dengue, ambayo imekuwa tatizo linaloongezeka wakati wa mvua.

“Ugonjwa huu huenezwa na mbu aina ya Aedes, mwenye mwili mweusi na madoa meupe, na huuma hasa wakati wa asubuhi, alasiri, na jioni.

Amesema dalili zake ni homa kali, maumivu ya viungo na misuli, uchovu, na maumivu nyuma ya macho zinafanana sana na malaria.

“Wananchi wanahimizwa kuondoa maeneo ya kuzaliana kwa mbu karibu na nyumba, ikiwa ni pamoja na maji yaliyosimama,vyombo vilivyotupwa katika mifereji iliyoziba, na mimea iliyokua.

Amesema nchi imekuwa katika mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu ulioathiri mikoa yote
isipokuwa Kilimanjaro na Njombe.

“Kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja uliopita, nchi yetu haijapata mgonjwa wa Kipindupindu.

Amewataka waanchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa Kuchemsha maji ya kunywa au kutibu kwa dawa maalumu, Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutoka chooni, baada ya kumhudumia mtoto aliyejisaidia na kabla ya kumyonyesha mtoto.

“Kuosha matunda kwa maji safi, kuepuka kula vyakula vya baridi au vilivyoandaliwa katika mazingira yasiyo safi, Kujenga vyoo bora, Kuepuka uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kujisaidia, kutupa taka au kutiririsha
maji taka na Kutunza mazingira na kuepuka kutupa taka ovyo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button