FAINALI za michuano ya Ligi ya vijana chini ya miaka 17 nane bora zinaendelea Dar es Salaam, ambapo mapema leo zimepigwa mechi mbili.
Katika michezo hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa KMC,uliopo Mwenge, Yanga imeifunga TFF Academy mabao 4-0 wakati Azam imeichapa Mbeya City bao 1-0.