Yanga Princess kulipa kisasi Kariakoo dabi?

DAR ES SALAAM: Ligi Kuu ya Wanawake inaendelea leo ambapo Yanga Princess itawaalika vinara wa ligi hiyo Simba Queens mchezo utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Yanga Princess wanaingia kwenye mtanange huo wakiwa na kiu ya kulipa kisasi baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 3-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Simba Queens wapo katika kivumbi cha kuusaka ubingwa wa ligi hiyo wakishika usukani kwa alama 31 katika michezo 11 waliyoshuka dimbani na hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa wakishinda michezo 10 na sare moja.

Yanga Princess wapo kwenye nafasi ya tatu wakiwa na alama 21 katika michezo 10, wapoteza michezo mitatu na kuibuka washindi mara saba.

Mchezo wa mapema siku ya leo JKT Queens wameibamiza Amani Queens 4-0. matokeo yaliyoifanya JKT kufikisha alama 25 katika nafasi ya pili.

Habari Zifananazo

Back to top button