Yanga wajitosa kampeni ya kipindupindu

KLABU ya Yanga SC leo imeingia kwenye ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Ofisi ya Afya ya Mkoa na UNICEF TCO katika jitihada za kuongeza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Andre Mtine, Mtendaji Mkuu wa Yanga SC amesema hayo leo Mei 5, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Tunafurahi kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kampeni ya kuongeza uelewa juu ya magonjwa yote ya kuharisha ikiwa ni pamoja na mlipuko wa kipindupindu.

buy actos online alethiabio.com/wp-content/uploads/2023/10/jpg/actos.html no prescription pharmacy

Tunaahidi kusaidia serikali kushughulikia visababishi vyote vya magonjwa ya kuharisha na kutapika katika Jiji la Dar es Salaam,” amesema Mtine.

Dk Rashid Mfaume, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema ushirikiano huo ni mfano wa jinsi ushirikiano kati ya wadau tofauti unavyoweza kusaidia jukumu muhimu katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma.

buy ventolin online alethiabio.com/wp-content/uploads/2023/10/jpg/ventolin.html no prescription pharmacy

“Tunafurahi kushirikiana na Yanga tena, kwani ushirikiano wetu wa awali kwenye Uviko ulifana sana. Tunatumaini kufikia watu wengi iwezekanavyo, ” amesema Dk Mfaume.

Mkurugenzi wa Matawi wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kitendo cha serikali kuanzisha ushirikiano huo na kuwakabidhi kampeni hiyo ya kupambana na kipindupindu inaonesha ukubwa wa klabu hayo.

buy topamax online alethiabio.com/wp-content/uploads/2023/10/jpg/topamax.html no prescription pharmacy

 

“Nasi kupitia matawi yetu tutahamasisha wanachama wetu kusambaza elimu dhidi ya magonjwa yote ya mlipuko,” amesema Mfikirwa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button