Yas yajivunia mchango sekta ya kilimo

DODOMA; KUPITIA Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kati, Said Idd ameeleza namna Yas inavyochangia mageuzi ya sekta ya kilimo kupitia mawasiliano bora na ya kisasa kwa wakulima kote nchini.

Akinukuu ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa robo iliyoishia Juni 2025, Said alisema Yas imeendelea kuongoza kitaifa kwa ubora wa huduma za simu na intaneti, mafanikio ambayo yamekuwa yakirudiwa kwa miaka mfululizo.

“Tunajivunia kuwa Yas haijajikita tu kwenye huduma za mawasiliano na kifedha, bali ni daraja la fursa kwa mkulima. Kupitia teknolojia ya 4G na 5G iliyoenea nchi nzima, mkulima anaweza kupata taarifa sahihi za soko, hali ya hewa, ushauri wa kitaalamu, na kupitia huduma ya Mixx by Yas, kupokea malipo hata akiwa shambani,” alisema na kuongeza:

” Yas inaendelea kuwekeza katika ujenzi wa minara mipya na kuboresha iliyopo ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma mijini na vijijini jambo linalowawezesha wakulima kushiriki kikamilifu kwenye uchumi wa kidijiti.

“Katika dunia ya leo, mawasiliano si anasa ni zana ya msingi ya maendeleo ya kilimo. Yas imesimama bega kwa bega na mkulima kuhakikisha anapata mtandao wa uhakika ili kuongeza tija katika shughuli zake.”.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button