Marekani yaamua kutoza Afrika dhamana

MAREKANI : WIZARA ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kwamba raia kutoka Zambia na Malawi watalazimika kulipia dhamana ya dola 15,000 kuanzia Agosti 20 ili kupata vibali vya biashara au utalii.

Hatua hiyo ni sehemu ya mradi wa majaribio wa kupunguza watu kubaki nchini humo baada ya vibali kumalizika muda wake. SOMA: Tanzania, Marekani zashauriana changamoto za uhamiaji

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara hiyo, Tammy Bruce, fedha hiyo ya dhamana itarejeshwa kwa mwombaji endapo ataheshimu masharti ya kibali chake, ikiwemo kuondoka Marekani kabla ya muda wa vibali kuisha.

Hatua hiyo inalenga kudhibiti ongezeko la wahamiaji wanaoingia kwa visingizio vya kisheria lakini wanakiuka masharti. Malawi na Zambia ni miongoni mwa mataifa yenye uchumi dhaifu barani Afrika, na mara chache raia wake hutembelea Marekani.

Utawala wa Rais Donald Trump uliweka msingi wa sera hii kupitia kampeni ya kudhibiti uhamiaji haramu, ambayo bado inaendelea kufanyiwa kazi na serikali ya sasa.

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button