ZEC yataka kampeni za kistarabu

ZANZIBAR: MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi, amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kistarabu, kuepuka vurugu na kuachana na matumizi ya lugha za matusi na kashfa wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu.
Akizungumza leo, Agosti 27, 2025, wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika katika ofisi za ZEC Maisara, Mjini Zanzibar, Jaji Kazi amesema vyama vyote vina wajibu wa kuheshimu sheria na maadili ya uchaguzi katika kipindi cha kampeni.
Mkutano huo umehudhuriwa na wanasiasa, asasi za kiraia pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, ambapo Jaji Kazi alisisitiza umuhimu wa vyama kufuata ratiba ya pamoja ya kampeni, ikiwemo kuheshimu muda wa kuanza na kumaliza kampeni kama inavyotakiwa na sheria na kanuni za uchaguzi.
“Kipindi hiki cha kampeni, vyama vya siasa vinatakiwa kuwa makini ili kudumisha amani ya nchi kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Wito wangu ni kwa vyama vyote kuhakikisha vinafuata sheria, kanuni, miongozo na maadili ya uchaguzi, kufanya kampeni kwa amani na kuepuka lugha za chuki, uchochezi au vitisho,” alisema Jaji Kazi.
Aidha, Jaji Kazi amehimiza vyama vya siasa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi pamoja na wadau wengine kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, utulivu na huru.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… Y You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good eaning opportunity.tab for more detail thank you……..
For details check ——-⫸ http://www.join.money63.com
I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com