ZEC yatangaza ratiba uchaguzi Z’bar

ZANZIBAR; TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza rasmi kuwa ratiba ya Uchaguzi mkuu kwa upande wa Zanzibar ikiwemo uchaguzi wa mapema utakaofanyika Oktoba 28, 2025.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji George Joseph Kazi, amesema kura ya mapema ipo kisheria na kwamba uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa urais wa Zanzibar , uwakilishi na udiwani itaanza  Agosti 28 hadi 10 Septemba 2025 saa 10:00 jioni.

Amesema uteuzi wa wagombea utakuwa Septemba 11 saa 10:00 jioni na kampeni za uchaguzi zitakuwa Septemba 11 majira ya saa 10:01 jioni baada mgombea kuteuliwa na zitamalizika Oktoba 27 saa 12:00 jioni

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button