Zimebaki asilimia 5 uwanja wa Mkapa ukamilike

SERIKALI imesema zimebaki asilimia 5 kumaliza kwa ukarabati uwanja wa Mkapa.
–
Vyumba vinne vya wachezaji, sehemu ya kuchezea, vyumba vya waamuzi, afya na eneo la video za marejeo (VAR) vimekamilika.
–
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema ukarabati huo ni wa awamu ya kwanza na mpaka sasa umefikia asilimia 95 zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku tano kuanzia leo.
–
“Tayari taa za kisasa 320 za mfumo wa LED zimefungwa na kuna huduma ya mtandao wa bure kabisa kwa ajili ya watazamaji wa mechi ambao tutauzindua kati ya tarehe 17 hadi 19 mwezi huu kabla ya mchezo wa ufunguzi wa African Football League kati ya Timu ya Simba na Al Alhy ya nchini Misri tarehe 20,2023. “amesema Ndumbaro.
–
Akikagua ukarabati huo leo Oktoba 9, 2023, Dk Ndumbaro amesema katika eneo la watu mashuhuri na sehemu ya wandishi wa habari kazi iliyobakia ni ndogo ambayo itamalizika ndani ya siku hizo tano akiongeza kuwa mfumo wa sauti uwanjani tayari umerekebishwa.
–
Dk Ndumbaro amesema Kampuni ya Formula 360, itafunga mfumo wa matangazo kidijitali ambao utaanza kufanya kazi rasmi Oktoba 20, 2023 huku akisistiza kuwa baada ya mchezo huo, ukarabati mkubwa wa awamu ya pili utaendelea.



