Zitto ataka uchunguzi huru vitendo vya utekaji

DAR ES SALAAM; SERIKALI imeshauriwa kufanya uchunguzi huru ili kubaini na kukomesha matukio ya utekaji yanayoendelea nchini.

Zitto ameshauri hivyo leo Julai 2, 2024 kuhusu kuripotiwa tukio la kutoweka mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Edgar Mwakabela maarufu kama ‘Sativa’ anayedaiwa kutoweka Juni 23, 2024 na kupatikana Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya Katavi.

“Uchunguzi huru ufanyike, ili kukomesha matukio haya yaliyoanza kushamiri katika siku za hivi karibuni. Matukio haya yanaharibu taswira ya nchi yetu, yanaturudisha katika zama ambazo wengine tuliamini tumeshatoka,” amesema Zitto.

Advertisement

“Njia pekee ya kukomesha haya ni kufanyika uchunguzi huru na wa kina, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watu watakaohusika na matukio haya,” amesema Zitto na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilianza kusahaulika, ila vimeanza kurejea na kuzua hofu.