Mwenge watembelea miradi mitano Masasi

HALMASHAURI ya Mji Masasi mkoani Mtwara imetembelewa na mbio za Mwenge wa Uhuru na kukagua, kuweka Jiwe la Msingi miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 800.

Akizungumza leo Aprili 9, 2023 wakati akikabiziwa mwenge huo baada ya kumaliza mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Eliasi Ntiruhungwa amesema katika miradi hiyo mitatu itawekwa Jiwe la Msingi na miwili kutembelewa.

Alitaja miradi ambayo itaweekwa Jiwe la Msingi kuwa ni ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na mradi wa vijana wa ugugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Miradi mingine ni ujenzi wa barabara ya Tanesco-Yatima kiwango cha lami umbali wa kilometa 1.1, Zahanati ya Kijiji cha Machombe, mabanda ya rushwa, ukimwi, madawa ya kulevya, lishe, malaria na dawati la jinsia.

Akizungumza wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea kikundi cha vijana wajasiliamali wanaojishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa (Azimio la Umoja) kilichopo Kata ya Mtandi kwenye halmashauri hiyo, Mjumbe wa kikundi Elleno George ambae pia ni Katibu wa kikundi hi hocho amesema mradi umegharimu zaidi ya Sh milioni 14.

Amesema faida kubwa itayotokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kutoa lishe bora kwa Jamii, ajira kwa wanakikundi, kuchangia kuboresha utunzaji wa mazingira.

Naye Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Geofrey Mwambe amewataka wananchi wa halmashauri hiyo kutumia nafasi hiyo ya Mwenge wa Uhuru kuchangamkia fursa ya mikopo mbalimbali inayotolewana halmashauri kwa kufanya biashara kupitia vikundi na Mtu mmoja mmoja.

Kiongozi wa mbio wa mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameipongeza mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kutokana umekidhi vigezo kulingana na thamani ya fedha za mradi huo.

Aidha amewasisitiza Vijana na Jamii kwa ujumla kwenye halmashauri hiyo juu ya suala zima la elimu ya ujasiliamali kwa ajili ya kukuza uchumi wao “Elimu siyo tu kwenye makaratasi bali elimu utumike katika masuala mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi tuifanyie kazi kwa vitendo tutumie taaluma na uwezo tuliyonao kushiriki vizuri kwenye miradi ya maendeleo ili kujikwamua kiuchumi”,amesema Kaimu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button