TAAISI ya Kiislamu ya Al- Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 50 ambao wanahitaji kuoa.
Akizungumza katika mashindano ya 23 ya kimataifa ya uhifadhi wa Qur’an ambayo yamefanyika leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Nurdin Kishki amesema kuwa mahari hiyo haitawahusu wale wanaotaka kuongeza mke wa pili.
Kishki amesema sharti hilo limewekwa kwa asiye na mke na sio lengo lake kusaidiwa wanaotaka kuongeza mke wapili.
“Tutafanya ndoa ya pamoja ya watu 50 mahari tutatoa Sisi Al-Hikma Foundation masharti usiwe unaongeza mke wa pili ndoa itafanyika Dar es salaam chini ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir”