4R za Samia zawavuta wasomi majimboni Geita

FALSAFA ya 4R ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imetajwa kuwavutia wasomi na wabobezi wa taaluma mbalimbali kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea ubunge katika majimbo mkoani Geita.
4R za Rais Samia zinabeba dhana ya maridhiano, ustahimilivu, marekebisho na ujenzi mpya wa muundo wa miundombinu, uchumi na taasisi imetajwa kuwapa wasomi wengi maono ya kuwania ubunge.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu ya kutia nia katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita, Mhandisi Kija Ntemi amesema dhana ya 4R imewapa nafasi ya vijana kujiamini ndani ya chama.
Mhandisi Ntemi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Wachimbaji wilaya ya Chato na mtia nia katika jimbo la Katoro amesema 4R za Samia zimeleta uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa chama na serikali.
Amesema kilichomvuta kutia nia ni kwa sababu anaamini chini ya misingi ya serikali ya awamu ya sita anayo nafasi ya kupata ridhaa na kutumia taaluma yake ya uhandisi kuisaidia CCM kutekeleza ilani.
Naye Katibu wa Kampuni ya Wanawake Na Samia Geita (WANASAGE), Alieth Ngaiza mwenye shahada ya Uzamili ya Mipango na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Jordan amesema ametia nia jimbo la Geita mjini.

Alieth amesema misingi ya utawala wa Rais Samia imewafundisha kuwa utawala si umaarufu bali ni hekima na busara na hivo anayo imani ataaminiwa na CCM kuwa miongoni mwa wagombea wa chama.
Kwa upande wake mbobezi wa jiolojia, Magembe Noni ambaye ametia nia jimbo la Geita mjini amesema yeye ni miongoni mwa watu walipata fursa ya usimamizi wa miradi ya kimkakati chini ya Rais Samia.

Magembe amewahi kuhusika kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme kati ya Tanzania-Zambia.
Amesema ana matumaini makubwa chini ya 4R za Samia kila mtu anaweza kupata nafasi na fursa ya uongozi na kwa kutumia taaluma yake ataweza kusaidia usimamizi wa 4R katika jimbo la Geita mjini.

Naye Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii na Utafiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dk Sadock Peter ambaye ni mtia nia jimbo la Busanda amesema 4R zimeleta mfumo shirikishi kwa makundi yote.
Dk Sadock ambaye ni Katibu wa Waganga Wafawaidhi Hospitali za Halmashauri, amesema anatamani kupata ridhaa ya CCM ili kutumia taaluma yake kusaidia kutafsiri kwa vitendo 4R katika jimbo la Busanda.

Mwalimu mwandamizi kwa miaka 25, mwenye shahada ya ualimu, John Udoya amesema amewiwa kutia nia jimbo la Geita mjini kwa sababu ya mfumo rafiki wa chama na serikali inayomfanya ajione ana nafasi.
Mwalimu John kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Geita anaamini muundo wa 4R ni nguzo kwa kila kiongozi kutekeleza, kusimamia na kufanikisha miradi ya kijamii.
Google pay 145$ dependably my last pay check was $8500 working 10 hours out of reliably on the web. My undeniably young family mate has been averaging 16k all through ceaseless months and he works around 24 hours dependably. I can’t trust in howdirect it was once I endeavored it out.This is my basic concern…HERE……… Www.JoinSalary.Com