NGULI wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Curtis James Jackson ‘50 Cent’ amekataa zaidi ya Sh bilioni 8 baada ya kutakiwa kutumbuiza kwenye moja ya mikutano ya Kampeni za Mgombea Urais wa Marekani Donald Trump.
Akizungumza katika mahojiano na kipindi Break Fast Club kinachorushwa na televisheni moja nchini humo, 50 Cent amekiri kuogopa kujihusisha na siasa na dini akihofia mgawanyiko wa watu na machafuko.
“Ni kweli nilipokea ofa ya kutumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa Trump kwenye ukumbi wa Madson Square Garden lakini nilikataa kwa sababu zangu hasa mashabiki zangu. Unajua naogopa sana siasa, ukijiingiza kwenye siasa lazima kuna wakukupinga waibuke, sio wote watakubaliana na wewe,”amesema 50 Cent.
Amesema dini na siasa ilimgombanisha Kanye West na baadhi ya mashabiki zake. “Kiufupi mimi sipendi siasa”, ameongeza 50 Cent.