53% wanufaika mkopo mfuko wa SELF

ARUSHA: SERIKALI kupitia Mfuko wa SELF imetoa mikopo ya Sh bilioni 397 na kuwafikia wanufaika 388,000 ambapo asilimia 53 ni wanawake.

Aidha wajasiriamali wadogo waliojikita katika kilimo, wafugaji, wajasiriamali na taasisi ndogondogo wamenufaika na mkopo huo.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Self, Santiel Yona wakati akiongea na waandishi wa habari katika kikao cha kumtambulisha Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Paul Sangawe

Amesema mfuko huo pia umewezesha kuzalisha faida ya Sh bilioni 4.73 ikiwemo kutoa gawio kwaserikali la sh, milioni 690.947 ya faida wanayozalisha.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sangawe amemshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kumteua kwa mara ya pili kuongoza mfuko huo katika kuhakikisha wananchi wa kipato cha chini wanaojoshughulisha na ujasiriamali ili kuwainua kiuchumi.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mfuko huo umeongeza mtaji kutoka Sh bilioni 58.47 na kufikia mtaji wa Sh bilioni 59.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button