PWANI: Zaidi ya Kompyuta 50 zimetolewa katika Shule mbili za Seekondari za Mwinyi Hassan Makumbura na Mfasiri Sekondari zilizopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani ili kukuza matumizi ya tehama katika shule hizo.
Akizungumza leo Afisa Tehama wa Wilaya ya Mkuranga,Kassim Mrutu wakati wa uzinduzi wa maabara ya kompyuta iliyofadhiliwa na Kampuni ya Songas kwa kushirikiana na Camara Education Tanzania amewataka wazazi na walezi kuwahamasisha watoto wao kujifunza mambo yanayofuata maadili ya kitanzania kupitia vifaa vya kielektroniki.
“Lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika wilaya hiyo,”ameeleza Mrutu.
SOMA: Vifaa vya kieletroniki mkombozi kwa walimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwinyi, Hassan Makumbura amebainisha kuwa shule hiyo kwa sasa ina wanafunzi zaidi ya 1,700 hivyo amewataka wadau nchini kuendelea kusaidia upatikanaji wa vifaa vya TEHAMA ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.
Naye Meneja wa Camara Education Tanzania Dayan Mbowe amebainisha kuwa lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu.
SOMA: https://www.ucsaf.go.tz/news/ucsaf-yakabidhi-vifaa-vya-tehama-kwa-baadhi-ya-shule-za-umma-nchini
Kwa upande wake Meneja wa miradi ya kijamii kutoka Songas Nicodemas Chipakapaka,amesisitiza kuwa ili kurudisha faida kwa jamii kampuni ya Songas imejikita katika miradi ya elimu, afya, mazingira pamoja na ukuzaji uchumi katika maeneo linapopita bomba la gesi asilia.