CANADA: Msanii wa filamu nchini, Rose Alphonce ‘Munalove’ amejifungua mtoto mwingine wa kiume baada ya kupitia maumivu na kejeli nyingi kufuatia kumpoteza mtoto wake Patrick, ambaye alifariki Julai 3,2018.
Muna Love ameweka picha akiwa na mtoto wake mchanga wakiwa Hospitali nchini Canada na kuacha andiko lililowagusa wengi huku akiomba ulinzi kwa mtoto wake.
“Asante Yesu kwanirudishia zaidi ya kile ulichochukua, nikisema nianze kuelezea matendo yako makuu juu yangu sitamaliza” amesema,
Aliongezea kuwa “Lakini sikuchoka Neno langu lilikua wakati nalia kwa uchungu ndani ikiwa mbele zao najikaza najifanya siumii nilikua nakuambia kwa uchungu wewe Yesu unajua ukweli unanijua niponye wewe Yesu” alimalizia.