Ndoto ya Nandy azae watoto 10

DAR ES SALAAM; WASANII wa bongo fleva William Lyimo ‘Billnass’ na Faustina Mfinanga ‘Nandy’ wametimiza miaka miwili ya ndoa, huku Nandy akisema ndoto yake ni kuzaa watoto 10.

Soma: Nandy: Lolote namshirikisha Bilnass

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy amefunguka kuwa ndoto yake ni kumzalia mume wake watoto 10: “Mume wangu miaka miwili ya ndoa yetu imekuwa fundisho kubwa kwangu, kujua upendo ni kitu muhimu sana, uwepo wako umerahisisha maisha yangu na ya kipenzi chako, nayajua tu tunakupenda sana.

Advertisement

“Nachokuomba najua wanaume mmeumbiwa kupepesa macho japo sio mwanaume wangu wewe (joke), popote uendapo, chochote ufanyacho jua una watu wanakupenda na kukuhitaji sana, kuyashinda majaribu now days ni rahisi sababu kila kitu kishapitwa na wakati na wakati wenyewe ndo sasa kuonesha mfano na kuwa mifano bora kwa watu wenye mapenzi ya kweli kuwa vijana wakiamua inawezekana.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

“Mungu wangu atulinde nitimize ahadi ya watoto wako 10. Nakupenda Billnass Happy Anniversary My Love, ”ameandika Nandy.