Syria kukabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni

SYRIA : WAZIRI mkuu mpya wa Syria Mohammed al-Bashir amewataka raia wote wa Syria wanaoishi nje ya nchi warejee nyumbani baada ya kuangushwa kwa serikali ya Bashar al-Assad.

Bashir  amesema serikali yake ya mpito itahakikisha inalindwa raia wote wa Syria na kuwapa huduma za msingi licha ya nchi hiyo kukabiliana na changamoto za ukosefu wa  sarafu za fedha za kigeni.

Hivi sasa Jumuiya ya Kimataifa,Umoja wa Ulaya wamepanga kukutana na kujadili mgogoro wa Syria mjini Berlin. SOMA: Mawaziri wako kazini kuimarisha usalama

Advertisement

Hatahivyo,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ambaye  ameelekea  Jordan na baadaye anataraji kwenda Uturuki kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.

Wakatihuohuo , Qatar imesema itafungua tena hivi karibuni ubalozi wake mjini Damascus baada ya serikali ya Syria kuangushwa..