Ujerumani , Nigeria kuimarisha uhusiano wa kibiashara

NIGERIA : RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu amemwambia Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier kwamba milango ya Nigeria iko wazi katika biashara.

Katika siku ya kwanza ya ziara ya Steinmeier katika nchi tatu za Afrika, Tinubu amesisitiza kuwa Nigeria imeanzisha mageuzi  makubwa  ya uchumi katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kupunguza urasimu na mageuzi ya kodi.

Akiwa mjini Abuja, Steinmeier amepongeza juhudi za Nigeria za kufanikisha mageuzi ya uchumi yatakayoleta tija katika mahusiano ya kibiashara. SOMA: Rais wa Ujerumani kufanya ziara Tanzania

Advertisement

Steinmeier amesema Nigeria yenye watu takribani milioni 220, ni mshirika wa pili kwa ukubwa wa kibiashara wa Ujerumani katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kabla ya kukutana na Tinubu, kiongozi huyo wa Ujerumani alikutana na Omar Touray, Rais wa Jumuia ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.