Rais wa Ujerumani kufanya ziara Tanzania

DODOMA: RAIS wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, atafanya ziara ya kikazi nchini kuanzia Oktoba 30 hadi 01 Novemba 2023.

Ziara hiyo mbali na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa

kimaendeleo baina ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kwenye kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

“Ujumbe wa Rais Steinmeier utajumuisha viongozi wengine wa serikali, pamoja na wawekezaji wa makampuni makubwa 12; utawasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, 30 Oktoba 30 2023 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,” imeeleza taarifa hiyo.

Akiwa nchini, Rais Steinmeier atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam, Oktoba 31, 2023. Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao watapata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea kuhusu masuala muhimu yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yao.

Marais hao watapata fursa ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara, litakalohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo mbili, lililoandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani kwa ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika Hoteli ya Hyatt Regency; ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao watapokea taarifa iliyojadiliwa na Jukwaa hilo.

“Siku ya tarehe 01 Novemba 2023, Mheshimiwa Rais Stenmeier atasafiri kwenda wilayani Songea, mkoani Ruvuma kutembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji na Shule ya Msingi ya Majimaji.

Hii ni makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonesha historia kubwa ya Vita vya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani,” imeeleza taarifa hiyo

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 60.

Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati hususan biashara na uwekezaji, maji, afya, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake, uhifadhi wa bioanuai, usimamizi wa fedha, utalii pamoja na malikale na utamaduni.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Tanzania imekuwa ikiuzia Ujerumani bidhaa zenye thamani ya wastani wa Dola za Marekani milioni 42.04 kwa mwaka. –

Bidhaa kuu ambazo Tanzania inaiuzia Ujerumani ni pamoja na kahawa, tumbaku, pamba, asali, samaki, nta na vito vya thamani.

Kadhalika, Tanzania inaagiza bidhaa kutoka Ujerumani zenye wastani wa Dola za Kimarekani milioni 237.43 kwa mwaka na bidhaa kuu zinazoagizwa kutoka Ujerumani ni Dawa, Vifaa Tiba, Mafuta (manukato, vipodozi) Magari, Vifaa na Mashine za Umeme.

Kwa upande wa uwekezaji, Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini. Kwa mujibu wa TIC hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.

Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imefanikiwa kusajili miradi 15 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300.00 ambayo imezalisha ajira 905.

Kampuni za Kijerumani zilizowekeza nchini zinajihusisha zaidi na sekta za kilimo, viwanda, nishati mbadala, ujenzi, utalii sanaa na utamaduni. Kufanyika kwa ziara hii ni ushahidi tosha kuwa Diplomasia ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inazidi kupaa

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Www.BizWork1.Com
1 month ago

Making additional money each month by performing a simple online task. Just by dedicating two hours a day to my home-based profession, I was able to earn and get $18,539 last month. Simple enough that even a youngster may learn how to do it and begin earning money online.
.
.
Detail Here———————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

AMIGO
AMIGO
1 month ago

Barua ya wazi kwa RAIS WA UJERUMANI Frank-Walter Steinmeier

Mabaki miili ya Watanzania kurudishwa nchini

“Baadhi ya mabaki hayo ni ya miili ya machifu na viongozi waliokuwa vinara katika vita vya Tanganyika dhidi ya Ujerumani (Maji Maji)”

= Mashujaa wa kuhamisha Makao makuu ya Tanzania pale Dodoma hoyeeeeee…
HAPA KAZI TU NA KAZI ZOTE HIZO IENDELEE SIO KAZI KWELI AU TUMEENDELEA SANA

Tanzania, Ujerumani kujadili kurejesha mabaki ya miili ya Watanzania walipoteza maisha wakati wa ukoloni

| JAMHURI MEDIA
https://www.jamhurimedia.co.tz/tanzania-ujerumani-kujadili-kurejesha-mabaki-ya-miili-ya-watanzania-walipoteza-maisha-wakati-wa-ukoloni/

Capture.JPG
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x