PALESTINA : Mabaki ya mwili wa mateka yapatikana

PALESTINA : MWILI wa raia wa Israel aliyeshikiliwa mateka na wanamgambo huko Gaza tangu shambulizi la Oktoba 7, umetambuliwa baada ya mabaki yake kupatikana.
Kutokana na uchunguzi wa kitaalamu, jeshi la Israel limesema leo kuwa limeiarifu familia ya Hamza al-Zayadna kwamba aliuawa wakati akishikiliwa mateka na Hamas.
Siku ya Jumatano, jeshi lilitangaza kuwa mwili wa baba yake, Hamza Youssef, uligunduliwa na ulirudishwa Israel. SOMA: Usitishaji vita Israel, Hamas bado kitendawili
Wawili hao walikuwa sehemu ya mateka zaidi ya 200 waliochukuliwa na wanamgambo wa Kipalestina kutoka Kibbutz Holit karibu na mpaka wa Gaza, wakati wa shambulizi baya dhidi ya Israel, Oktoba 2023.
Mapigano kati ya Israel na Hamas yamesababisha mauaji ya watu 46,000 huko Gaza, wengi wao wakiwa ni raia.