Sita jela miaka 3 kuchoma moto basi la Saibaba

MAHAKAMA ya wilaya ya Korogwe imewahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh milioni moja kila mmoja watu sita walioshitakiwa kwa tuhuma za kuhusika na kuchoma moto basi mali ya kampuni ya Saibaba kinyume na sheria.
Akisoma shitaka hilo mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Francisca Maguiza, Mwanasheria wa Serikali Sarah Wangwe amesema washtakiwa hao walitenda kosa la hilo Februari 17, 2024 katika eneo la Shamba Darasa, Kijiji cha Msambiazi kata ya Mtonga wilayani Korogwe.

Waliokutwa na hatia ni Bashiru Shehoza, Bakari Anania, Bakari Mhando, Ramadhani Malaba, Benjamin Shehoza na Abdallah Koko wote wakazi wa Korogwe.
Hata hivyo, Hakimu Maguiza amesema watuhumiwa hao wana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 au kuendelea kutumikia adhabu hiyo.



