Makalla: Ilani mpya ya CCM yabeba matumaini ya Watanzania

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla amesema Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka 2025-2030 imebeba matumaini makubwa kwa Watanzania kwani inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi na changamoto zinazowakabili.

Makalla ameeleza hayo wakati akisalimia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Arusha Mjini kuendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Alisema ilani hiyo mpya imetokana na tathmini ya ilani iliyopita, kupitia mchakato wa utafiti, ushirikishwaji wa wananchi, asasi za kiraia na wadau ili kubaini mahitaji halisi na vipaumbele vya taifa.

“Ilani hii imeandaliwa kwa kushirikisha wananchi, hivyo inakwenda kushughulikia masuala ya ajira, uchumi, miundombinu na changamoto zote zinazowakabili Watanzania,” alisema Makalla na kuongeza kuwa muda ukifika CCM itaanza kuinadi kwa sababu ni ilani ya wananchi.

“Inahusu mustakabali wa maisha ya Watanzania, na hakuna chama kingine chenye ilani bora zaidi ya CCM,” alisisitiza.

Makalla pia alikiri kuwepo kwa changamoto kadhaa licha ya mafanikio yaliyopatikana, na kusema CCM ina dhamana ya kuzitatua.

Alitolea mfano changamoto ya maji Arumeru Magharibi na kueleza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso atakwenda huko baada ya kumaliza ziara yake Karatu ili kushughulikia tatizo hilo.

“Nataka niwahakikishie kuwa changamoto za Watanzania hazina mbadala, ni CCM pekee yenye uwezo na
dhamira ya kweli kuzitatua,” alisema Makalla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button