Vifo vya wasanii vilivyotikisa mwaka 2025

MWAKA 2025 ulianza kwa furaha kwa baadhi ya mastaa wakifunga ndoa, kupata watoto na kushuhudia mafanikio mbalimbali. Hata hivyo, furaha hiyo iligeuka kuwa majonzi makubwa baada ya tasnia ya burudani na michezo kupoteza wasanii na wadau wake muhimu waliotoa mchango mkubwa kuelimisha, kuburudisha na kuijenga jamii ya Watanzania.
MC Pilipili aaga dunia
Miongoni mwa waliotikisa vichwa vya habari ni kifo cha msanii, mwalimu, mchungaji na mshehereshaji mashuhuri Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’. MC Pilipili alizaliwa Oktoba 1, 1985 mkoani Dodoma. Mbali na kuwa mshehereshaji, pia aliwahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuamua kutumia kipaji chake cha uchekeshaji na kuhubiri Injili.
Alifariki dunia Novemba 16, 2025 mkoani Dodoma, akiwa na umri wa miaka 40. Taarifa ya Polisi ilieleza kuwa alikutwa na majeraha mbalimbali mwilini mwake. Mazishi yake yalifanyika Novemba 20, 2025 katika makaburi ya Kilimo Kwanza, Dodoma. MC Pilipili ameacha mjane na watoto wawili.

Hawa Hussen ‘Carina’
Tasnia ya filamu ilikumbwa na pigo kubwa baada ya kufariki kwa muigizaji Hawa Hussein ‘Carina’ Aprili 15, 2025 nchini India, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa tumbo, baada ya kupelekwa nchini humo Februari 24, 2025.
Mwili wa marehemu uliwasili nchini Aprili 18, 2025 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na alizikwa Aprili 19, 2025 katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Ameacha mtoto wa kike, Aisha, mwenye umri wa miaka 16.
Carina anakumbukwa zaidi kama Video Queen wa wimbo Oyoyo wa Bob Junior na kwa kuigiza katika tamthilia Kiu ya Kisasi (2017–2018) ya Jacob Stephen ‘JB’.
Hashimu Lundenga
Huzuni nyingine ilitanda baada ya kufariki kwa aliyekuwa mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga, Aprili 19, 2025 jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua maradhi ya kiharusi kwa muda mrefu.
Lundenga alisimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia mwaka 1994 hadi 2018 na ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuyafanya mashindano hayo yajulikane ndani na nje ya nchi. Alizikwa Aprili 22, 2025 katika makaburi ya familia Kidatu, mkoani Morogoro.

Omari Seseme
Mei 12, 2025, muziki wa dansi uliingia majonzini baada ya kufariki kwa mpiga gita mkongwe wa bendi ya Sikinde, Omari Seseme kutokana na maradhi ya moyo . Seseme pia amepata kutamba na dendi ya African Revolution ‘Tamtam’ , Double M Sound ‘Mshikemshike’ na Super Kamanyola ya Mwanza. SOMA: Buriani Peter Mwenda, umetuachia hazina
Raidanus Vitalis ‘Kitundu’
Juni 24, 2025, tasnia ya tamthilia ilimpoteza muigizaji wa Jua Kali, Raidanus Vitalis ‘Kitundu’, aliyefariki Hospitali ya Temeke alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya kifua na tumbo. Alizikwa Juni 26, 2025 katika Makaburi ya Wailes, Temeke. Mbali na uigizaji, marehemu alikuwa na vipaji vya uimbaji na dansi, na aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali kama vile Vanessa Mdee, Chino Kidd na Rich Mavoko.
Mzee Ally Samatta baba
Sekta ya michezo ilikumbwa na pigo baada ya kufariki kwa Ally Samatta, baba wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, Julai 6, 2025 nyumbani kwake Mbagala, Dar es Salaam, alizikwa Julai 7, 2025 Kibiti, mkoani Pwani.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com