Zanzibar yaahidi miundombinu ya kisasa kwa wawekezaji

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaendelea na dhamira ya kuweka miundombinu ya kisasa kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kuzitumia fursa za biashara ipasavyo.
Ameyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho Dimani Wilaya ya Magharibi B Unguja. Amesema maonesho hayo yamekuwa ni nguzo muhimu inayounganisha sekta ya biashara na huduma nyingine zikiwamo taasisi za serikali na binafsi, kampuni, wajasiriamali, wafanyabiashara, wawekezaji na wazalishaji wa ndani na nje ya nchi.
“Majukwaa ya biashara kama haya ni fursa kwenu ya kujiendeleza na kukuza biashara kwenu na taifa. Pia hapa mtajifunza mambo yanayohusiana na biashara, kuimarisha viwango vya bidhaa kulingana na mabadiliko ya teknolojia, niwasihi washiriki wote mtumie vyema nafasi hii kwa kukuza masoko,” alisema Abdulla.

Amesema Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda kupitia maonesho hayo imeweka wazi uwekezaji katika biashara na viwanda kwa kuongeza fursa a vituo vya za uwekezaji kwenye sekta za utalii, biashara, viwanda, kilimo na uchumi wa buluu. SOMA: Rais Mwinyi afungua flyover iliyopewa jina lake
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu, Mudrik Ramadhan Soraga amesema shabaha ya serikali ni kuhakikisha wanaendelea kuyapa hadhi kubwa maonesho hayo ya biashara ili yakidhi vigezo vyote vya matamasha na maonesho ya kimataifa.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Dk Habiba Hassan Omar amesema lengo kuu la kufanyika kwa maonesho hayo ni kukuza biashara. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC), Ali Amour Suleiman alieleza kuwa biashara na ubunifu ndio nguzo inayoweza kuifanya biashara kukua, kuimarika na kuleta tija kwa wafanyabiashara na taifa kwa ujumla.




l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Payathome9.Com