Rais Samia: Amani ndio nguzo ya uwekezaji

ZANZIBAR; RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kukua kwa uwekezaji nchini kumewezekana kutokana na uwepo wa amani na utulivu wa kisiasa, na kuwataka wanaochochewa kuvunja amani kuacha mara moja.
Aidha, amesisitiza wananchi kulinda amani ya nchi, kwani maendeleo na kupeN deza kwa nchi kunatokana na amani na usalama uliopo.
Rais Samia alieleza hayo jana Zanzibar, alipokuwa akizundua Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyojengwa Unguja.
“Tusisahau kwamba kukua kwa uwekezaji nchini kunawezekana kutokana na uwepo wa amani, usalama na utulivu wa kisiasa. Sasa kwa wale wanaochokorewa masikio kuvunja amani ya nchi hii, ni wasihi acheni mara moja kwani amani ikichafuka haichagui,” alieleza Rais Samia.
Alieleza kuwa tofauti za mawazo zipo lakini hazipaswi kuwagawa wala kuwafanya kuharibu utulivu na amani.
“Nilikuwa nazungumza na mwekezaji hapa, hoteli ny ingine mbili atazifungua lakini akaninong’oneza kuna eneo kama ameshachukua, hajajenga lakini bado ameuliza maeneo mengine kama yapo. Huyu ni mmoja lakini wawekezaji wa aina hii wapo wengi, wana vutwa kwetu kwa usalama amani na utulivu wa nchi yetu,” alisema.
Rais Samia alisema sekta ya utalii nchini imeendelea kuimarika ambapo kuanzia mwaka 2022 hadi 2025, imeajiri zaidi ya Watanzania milioni 2.5 na idadi ya watalii wa nje na ndani iliongezeka hadi kufikia 5,360,247, ikilinganishwa na watalii 1,409,800 mwaka 2020.
“Kwa Zanzibar pekee, idadi ya watalii wanaokuja imeongezeka kutoka 743,606 mwaka 2024 hadi 816,000 mwaka jana na matarajio yetu na mambo haya yanayofungu liwa, idadi ya watalii itaendelea kuongezeka kuja kwetu Zanzi bar,” alisema.
Aliongeza kuwa mchango wa sekta ya utalii kwenye pato la serikali kwa Zanzibar ni zaidi ya asilimia 30. Alisema idadi ya ho teli zinazofanya kazi visiwani humo hadi kufikia mwaka jana imefikia 400.
“Niwapongeze Kampuni ya Reliance Resort and Tourism Limited kwa uwekezaji huu mkubwa wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 135, ni uwekezaji mkubwa haujapata kutokea Zanzibar.
Hadi sasa, mradi wa ujenzi wa hoteli hii umefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 158 kwa Watanzania wengi, wakiwa vijana wa Michamvi,” alifafanua.
Vilevile, Rais Samia alisisitiza kwamba katika uendeshaji, wahusika wahimize matumizi ya bidhaa zinazoza lishwa nchini na kwamba kazi ya wawekezaji ni kuwekeza na kuendesha shughuli za hoteli lakini shughuli zingine kama kuongoza watalii, zinapaswa kubaki kwa wenyeji.
“Niwahakikishie wawekeza ji wote kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuweka mazingira rafiki na miundombinu wezeshi ili kuvutia wawekezaji wenye tija kama huyu,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Sharif Ali Sharif alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana Zanzibar ni pamoja na kuongezeka kwa miradi ya kimkakati ambayo imeongeza ushindani chanya, ubora wa huduma na hadhi ya Zanzibar katika soko la utalii la kimataifa.




l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Payathome9.Com