Ulega azungumzia mikopo kwa maendeleo ya taifa

DODOMA: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema Serikali imekuwa ikikopa mikopo nafuu kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya kisasa ya barabara na viwanja vya ndege nchini, akisisitiza kuwa mikopo hiyo imeleta matokeo makubwa yanayoonekana kwa wananchi.
Akichangia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/2027 bungeni, Ulega alipinga kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa upinzani kwamba Serikali inaendelea kukopa bila kutekeleza miradi ya maendeleo, akizitaja kauli hizo kuwa za uzushi na zinazolenga kuwachonganisha wananchi na Serikali.
“Nataka niwaambie kwamba hakuna fedha zilizokopwa ambazo zimeshindwa kuleta maendeleo. Kwa upande wa Wizara ya Ujenzi, ushahidi wa matumizi ya mikopo hiyo unaonekana wazi,” alisema Ulega.
Alimpongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuimarisha miundombinu nchini, akieleza kuwa mikopo nafuu imewezesha ukarabati na uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Tabora, Shinyanga, Sumbawanga, Kigoma, Tanga na Manyara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Ulega alisema mafanikio hayo yanaonekana pia katika sekta ya usafiri wa anga, ambapo hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi amekuwa akiruhusu safari za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), katika baadhi ya viwanja vya ndege vilivyokamilika hatua inayolenga kuchochea uchumi na kurahisisha usafiri wa wananchi.
Aidha, alisema Serikali inaendelea na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, ambao unatarajiwa kuwa kitovu kikubwa cha usafiri wa anga nchini na ukanda wa Afrika Mashariki kwa kupokea ndege kutoka mataifa mbalimbali.
Katika upande wa barabara, Ulega amesema mikopo hiyo imewezesha kuanza kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Chamwino Ikulu hadi Jiji la Dodoma, pamoja na maendeleo ya mji wa kisasa wa Serikali katika makao makuu ya nchi.
Kwa upande wa Mkoa wa Kigoma, Waziri huyo alisema mikopo nafuu imechangia kukamilika kwa miradi muhimu ya barabara ikiwemo Malagarasi–Uvinza na Kasulu–Manyovu, ambayo imeimarisha usafiri na shughuli za kiuchumi.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
.
More Details For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com